China yarusha chombo cha kuchunguza sayari ya mwezi Chang'e No. 3



China leo alfajiri imerusha chombo cha kuchunguza sayari ya mwezi Chang'e No. 3 yenye kigari kidogo cha kwanza cha kufanya uchunguzi kwenye sayari ya mwezi. Chombo hicho kimerushwa saa 7 na nusu usiku kwa kutumia roketi ya aina ya Long March-3B kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Xichang, kusini magharibi mwa China. Hii ni mara ya kwanza kwa China kurusha chombo cha anga ya juu kitakachotua kwenye sayari nyingine, na pia ni chombo cha kwanza cha kutua kwenye sayari ya mwezi kilichorushwa katika karne ya 21.

Chombo cha Chang'e No. 3 kinachoundwa na chombo cha kutua kwenye sayari ya mwezi na kigari kidogo cha uchunguzi, kimepangwa kutua kwenye sayari ya mwezi katikati ya Desemba. Majukumu ya kigari hicho ni pamoja na kuchunguza sura na hali ya kijioloji ya sayari ya mwezi, na kutafuta raslimali za asili.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company