Wajumbe wa jopo la marekebisho ya katiba,Misri
Polisi nchini Misri wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa rais wa Kiislam aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi kutoka viwanja vya Tahrir mjini, Cairo.
Mapigano hayo yamekuja wakati makubaliano ya marekebisho ya katiba yakipitishwa na jopo la kurekebisha katiba ya nchi hiyo.
Katiba hiyo iliyofanyiwa marekebisho inatoa madaraka makubwa kwa jeshi, ikiwa ni pamoja na kuwashitaki raia katika masuala fulani.
Katiba hiyo itapigiwa kura ya maoni ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka kesho.
Jopo hilo la marekebisho ya katiba ya Misri lenye wajumbe 50 limekamilisha rasimu ya mwisho baada ya kutumia siku mbili kupitia katiba hiyo ambayo ilipitishwa chini ya utawala wa rais wa zamani aliyeondolewa madarakani, Mohammed Morsi.
Kadhalika, muda wa uchaguzi umebadilishwa, kiasi kwamba haielezi ni uchaguzi kati uanze kati ya ule wa wabaunge au rais
Rasimu ya kifungu cha 247-kinataka uchaguzi wa kwanza ufanyike katika kipindi cha siku 90, tangu kufanyika kwa kurta ya maoni.KIfungu hicho pia kinasema, uchaguzi mwingine ufanyike katika kipindi cha kufikia miezi baadaye.
Mwenyekiti wa jopo hilo amesema rasimu ya katiba itakabidhiwa kwa rais wa mpito Adly Mansour, Jumanne.
Rasimu hiyo pia inasema wanawake na Wakristo lazima wapate "uwakilishi mzuri" lakini ikisema sheria hiyo ya baadaye lazima itoe maelezo zaidi.
Katiba mpya inayopendekezwa itahitaji marais kutangaza mali zao, na kuruhusu wabunge kupiga kura ya kumtoa madarakani rais aliyechaguliwana kuitisha uchaguzi wa mapema ikiwa watafikia theluthi mbili ya wabunge wote.
Viwanja vya Tahrir ndipo ulipoasisiwa uasi uliomng'oa madarakani rais wa miaka mingi nchini Misri Hosni Mubarak miaka mitatu iliyopita.