Waziri mkuu wa Somalia atolewa madarakani.

Waziri mkuu aliyetolewa madarakani wa Somalia Abdi Farah.
Bunge la Somalia limepiga kura kumfukuza kazi waziri mkuu wa nchi hiyo na kumaliza mwaka mzima wa uthabiti wa nadra uliokuwa kwenye uongozi wa juu wa nchi hiyo.

Waziri mkuu Abdi Farah Shirdon alipoteza kura ya kutokuwa na imani kwenye bunge Jumatatu kwa jumla ya kura 184-65. Hakuna mtu aliyetajwa mara moja wa kuchukua nafasi yake.

Rais Hassan sheikh Muhamed alitaka Bw.Shirdon kujiuzulu miezi mitatu iliyopita kwa kudai kuwa hatendi kazi yake vyema.Waziri mkuu huyo alikataa wito huo na kulitaka bunge kuingilia kati.

Rais na waziri mkuu waliingia madarakani zaidi ya miezi 12 iliyopita kama sehemu ya mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kuipa Somalia serikali iliyo na thabiti baada ya zaidi ya miongo miwili ya ghasia na vurugu.

Bw.Shiron alikuwa ni mgeni katika siasa wakati huo akiwa ameshafanya kazi kama mfanyabiashara huko Kenya.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company