JUWA JINSI YA KUZUIA WATU WASIFUNGUE AKAUNTI YAKO YA FB AU EMAIL HATA KAMA WANA PASSWORD YAKO

Kuna wakati hata kama mtu anayo PASSWORD yako ya FB au akaunti yako ya barua pepe bado hawezi kuingia kwa akaunti yako.
Unaweza dhibiti watu wengine wasifungue akaunti yako ya email au Facebook kwa kufuata huduma ya ku sign in mara mbili.
Yaani ipo hivi:
1. Mara ya kwanza una sign in kama kawaida kwa kutumia ID na PASSWORD yako, ambapo hivi ndio umekuwa ukifanya wakati wote.
Ila kwa huduma hii ya kusign mara mbili, ID na PASSWORD pekee hazikuruhusu kuingia kwa akaunti yako.
2. Utakapomaliza ku sign in , utatakiwa kufuata hatua ya kuweka CODE maalum ambayo utatumiwa kwa njia ya ujumbe mfupi kwa simu yako. Au la pengine tayari ulipojiandikisha kwa huduma hiiya kusign mara mbili, basi uliweza ku download CODES maalum ambazo ni wewe tuu ndio utaweza kuzitumia.
---Fuata maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii ya kusign mara mbili kwa kubofya link hapo chini.

HUDUMA YA FACEBOOK KUSIGN IN MARA MBILI ...BONYEZA HAPA

HUDUMA YA GMAIL KUSIGN IN MARA MBILI ........BOFYA HAPA

HUDUMA YA YAHOO KUSIGN IN MARA MBILI .......BOFYA HAPA
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company