Kipa huyo Muargentina alitunguliwa na Toby Alderweireld aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Jose Sosa, hilo likiwa bao la kusawazisha baada ya Samuel kutangulia kuwafungia wageni dakika ya 65.
Atletico iliyomkosa mfungaji wao bora, Diego Costa, ambaye ni majeruhi sasa ina kazi ya kupambana na Barcelona hadj mwisho kuwania taji.
Barcelona inaendelea kushika nafasi ya pili kwa pointi zake 86 za mechi 37, nyuma ya Atletico yenye pointi 89 za mechi 37 pia, wakati Real yenye 84 za mechi 37 ya tatu.

Mmeniangusha vijana: Kocha wa Atletico, Diego Simeone akilalamika wakati wa mechi
