Duru za usalama nchini Misri zimearifu kuwa, watu wawili wameuawa na wengine kujeruhiwa, kufuatia mripuko wa bomu uliotokea katika medani ya Al-Mahkamah katika eneo la Misrul-Jadid mashariki mwa mji wa Cairo. Habari zinasema kuwa, mripuko huo umetokana na bomu la kutengenezwa nyumbani na kwamba umetokea karibu na idara ya usalama barabarani karibu na mahakama ya eneo hilo. Hayo yanajiri katika hali ambayo askari wengi wa usalama wamewekwa katika maeneo yote ya jirani na ikulu ya al-Ittihaadiyyah kuzuia hujuma yoyote ya waandamanaji. Hatua hiyo imekuja kufuatia wito wa viongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya kuitisha maandamano makubwa dhidi ya serikali ya nchi hiyo inayopata uungaji mkono wa jeshi. Hapo jana Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Misri Nabil Fahmy, alinukuliwa akisema kuwa, harakati ya Ikhwanul Muslimin itachukua kipindi cha miaka mingi kabla ya kurejea kwenye ulingo wa kisiasa nchini humo. Fahmy alisema kuwa, ni suala lililo mbali kuiona harakati hiyo ikirejea haraka katika ulingo huo, kutokana na idiolojia waliyonayo viongozi wake.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago