Jeshi la Iraq lawaangamiza magaidi 500 wa kigeni

Jeshi la Iraq likilinda doria nchini humo
Kamanda wa jeshi la Iraq amesema kuwa, mamia ya magaidi kutoka nje ya nchi hiyo wameangamizwa kwenye operesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi la nchi hiyo katika kipindi cha miezi mitano iliyopita magharibi mwa Iraq. Rashid Falih Kamanda wa Operesheni za kijeshi katika mkoa wa al Anbar, magharibi mwa Iraq amesema kuwa, wanamgambo wa kigaidi wasiopungua 500 kutoka mataifa mbalimbali ya kigeni waliangamizwa katika maeneo tofauti ya mkoa huo. Kamanda Rashid Falih ameongeza kuwa, AbdulRahman al Hayti kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh aliuawa jana kwenye operesheni za jeshi la serikali katika jimbo la Babil lililoko katikati mwa Iraq. Jeshi la Iraq limefanikiwa pia kuwatia mbaroni wasaidizi wawili wa AbdulRahman al Hayti na kuzinasa nyaraka mbalimbali zinazoonyesha harakati za kundi hilo katika mikoa ya al Anbar, Swalahuddin, Baghdad na maeneo mengine. Inafaa kuashiria hapa kuwa, zaidi ya magaidi 2,500 wameshauawa tokea serikali ya Iraq ichukue uamuzi wa kupambana na makundi ya kigaidi katika mikoa mbalimbali nchini humo yapata miezi mitano iliyopita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company