Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichogharimu kiasi cha bilioni 61.5 za kitanzania, ambapo alipongeza mradi huo kwani utasaidia kuondoa ugonjwa wa malaria nchini, pia aliipongeza sekta ya afya kwa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na malaria kwa asilimia 71 na wagonjwa wenye kuugua malaria kwa asilimia 51 kwa kipindi cha mwaka 2004-2014 leo Mjini Kibaha.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo aliipongeza serikali ya Tanzania katika kutekeleza Mradi huo utakaosaidia katika kupambana na vita dhidi ya malaria nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla, leo Mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo alishukuru na kupongeza uzinduzi wa kiwanda hicho kwani kitakuwa ni mwarobaini katika mapambano dhidi ya malaria kwa mkoa wa pwani na afrika kwa ujumla,leo Mjini Kibaha.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Abdalah Kigoda akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria na kuahidi kushirikiana kwa karibu na shirika la maendeleo ya taifa (NDC) katika kutekeleza majukumu ya kiwanda hicho ili kutekeleza agizo la Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika vita dhidi ya malaria kupitia Mradi huo, leo Mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant mzindakaya akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakifungua jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wakati wa Halfa ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani, Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Balozi wa Cuba nchini Tanzania Bw. Jorge Luis Lopez akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Cuba na Tanzania, ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika masuala balimbali ya maendeleo leo mkoani Pwani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.(Picha na Freddy Maro).
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete amesemaSerikali ina mpango wa nchi nzima wa kupulizia dawa kwa ajili ya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria lengo ikiwa ni kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Dokta Kikwete ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichopo eneo la TAMCO wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Raisi Kikwete alisema Serikali imekua ikipambana na ugonjwa huo kwa kutumia dawa za malaria za Mseto na baadae Vyandarua vyenye dawa za kuua wadudu wa ugonjwaambavyo vilisambazwa kwa nchi nzima huo lakini bado haijafanikiwa kuuondosha kabisa hapa nchini pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika.
Alisema Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia 10 mwaka 2012, ambapo pia idadi ya wagonjwa imepungua kutoka asilimia 51na vifo vimepungua hadi asilimia 71 kutoka mwaka 2004 hadi 2014..
Aidha Dokta Kikwete aliwataka wananchi kuendelea kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huo na kuondokana na dhana potofu kuwa vyandarua hivyo vinasababisha madhara hususani kwa wamnaume.
Kwa upandewake Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda alisema mikakati ya serikali ni kuongeza viwanda mama kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza kasi ya ugonjwa wa malaria ambao umekua kikwazo cha maendeleo kwa wananchi.
Waziri huo pia alibainisha kuwa Serikali ina mikakati ya kufufua bandari za nchi kavu na majini ikiwa sambamba na kuboresha miundombinu ya reli ili kuwezesha kufika kwa urahisi kwenye maeneo ambayo yalikua vikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kujenga viwanda na kuongeza fursa mpya ya ajira kwa watanzania hususani vijana ambao wataongeza pato la Taifa.
Waziri Mkuu wa Ethiophia na mwenyekiti wa kupambana na malaria barani Afrika HaileMariam Desalegn ataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo inaendelea kwa nchi za Afrika.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Christopher Mzindakaya alisema kuwa hadi sasa kiwanda hicho kimewaajiri wafanyakazi 145 na kimegharimu kiasi cha shilingi bilion 61.5 hadi kukamilika kwake pia kitakua na uwezo wa kuzalisha lita za ujazo milioni sita kwa mwaka.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago