Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga na kukosoa vikali ripoti ya kila mwaka ya Marekani kuhusiana na ugaidi na kusema kuwa, madai eti Iran inafadhili ugaidi duniani ni porojo tupu na upotoshaji wa ukweli wa mambo. Msemaji wa wizara hiyo, Bi Marzieh Afkham amesema leo kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa muhanga mkubwa wa hujuma na mashambulizi ya kigaidi kwa takriban miongo mitatu mfululizo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hapo jana imetoa ripoti yake ya kila mwaka kuhusiana na ugaidi ambapo imedai eti Tehran imezidisha uungaji mkono kwa makundi yanayodaiwa kuwa ya kigaidi huko Palestina, Bahrain na Yemen. Ripoti hiyo aidha imedai kwamba Iran imejipenyeza zaidi barani Afrika kwa lengo la kuvuruga amani ya dunia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kwamba Marekani ndiyo muungaji mkono mkubwa wa ugaidi duniani na kwamba kuisingizia Iran kuhusiana na hilo ni upotoshaji wa ukweli wa mambo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago