Kahama. Mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Majengo, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga amelazwa katika Hospitali ya wilaya baada ya kunusurika kifo kutokana na jaribio la kuchinjwa na baba yake mzazi.
Tukio hilo limekuja siku 10 baada ya mtu mmoja, Ustadh Mohamed Kurangwa (36), kumuua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nzasa, Jamal Salum (12) kisha naye kuuawa, Mbagala, Dar es Salaam.
Kurangwa alimuua Jamal nyumbani kwake Mbagala Charambe Mianzini kwa kumchinja na kuweka kichwa cha marehemu kwenye miguu ya mtoto huyo, kisha kuupeleka mwili wake choo cha nyumba anayoishi muuaji. Muuaji huyo alizoa damu na kuijaza kwenye ndoo kisha kuiweka pembeni ya nyumba yake kabla ya kuingia chumbani kwake, kujifungia na kusoma Koran. Katika tukio la Kahama, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Joseph Fwoma alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Said Siraji (13) na alifikishwa hospitalini hapo jana alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria mwema akivuja damu shingoni.
Imechapishwa na
Unknown